Marketing Manager for Harusi Trade Fair explaining to the press concerning Harusi Trade Fair 2012 at Maelezo Posta Dar-es-salaan on 23rd-March-2012
--
Kwa awamu ya tatu maandalizi ya maonyesho ya Harusi yanayotarajia kufanyika tarehe 30 machi hadi 1 april katika ukumbi wa Diamond Jubilee yatakua na washiriki na wadau mbalimbali waliobobea kwenye maswala ya Harusi pamoja na mahitaji yote ya Harusi.
Muanzilishi na muandaaji wa maonyeshao haya ya kila mwaka Mustafa Hassanali alisema“ Maonyesho ya mwaka huu yatakua makubwa sana kulinganisha na ya mwaka jana na tunatazamia kuyafanya maonyesho haya ya Harusi kuwa maonyesho makubwa nchini kote miaka ijayo”.
Ukweli katika nukuu, Maonyesho haya ya Harusi yalowavutia zaidi ya wafanya maonyesho 40 waliothibitisha ushiriki wao,wengi wakiwa waliwahi kushiriki katika miaka iliyopita ,wameweza kuona ukuaji katika maonyesho haya..
“ Harusi inaleta umoja katika familia na jamii na ni moja kati ya nyakati pekee zinazotokea katika maisha,hivyo mpango wetu ni kutoa mahitaji ya bibi Harusi na bwana Harusi katika sehemu moja na huu ni wakati muafaka wa wao kujipatia uzoefu katika bidhaa na huduma zote harusi,” alisema meneja masoko Hamis K Omary.
Maonyesho ya Harusi yanaleta pamoja wadau na wachuuzi mbalimbali waliobobea katika maswala ya Harusi na kufanya maonyesho haya kuwa na kiwango na uhakika nchini Tanzania. Kati ya wachuuzi mbalimbali watakaoshiriki mwaka huu ni wachuuzi wa keki, maua, wapiga picha, gauni za harusi, tovuti za wabunifu wa harusi, pamoja ubunifu mbalimbali unaousiana na maswala mazima ya harusi.
Mmoja kati ya washiriki katika maonyesho y Harusi 2012, ni Gabriel Makupa wa GRM productions, ambae ni mtayarishaji maarufu wa picha mbalimbali za Harusi. “ Tumepata uzoefu mzuri kwa mwaka ulopita ulotusaidia kupata wateja na nafasi ya kukuza biashara. Tulitangaza bidhaa na huduma zetu na kukuza idadi ya wateja kwenye maonyesho ya Harusi 2010 na ndio maana tunashiriki kuanzia kipindi hicho.
Kuna nafasi chache tu ambazo zinapatikana katika maonyesho ya mwaka huu.“Mpaka sasa makampuni 40 yanayohusika na maswala mbalimbali ya Harusi yamedhibitisha ushiriki wao na tunatarajia idaidi ya washiriki kuongezeka.So far 40 wedding related. Mwaka huu tuna bidhaa mpya kabisa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ili na wao waweza kukua.kwa hivyo tunawaomba wale wote wanaohusika na maswala ya Harusi kushiriki katika maonyesho haya ya Harusi” alimalizia Bw. Omary
Ikiwa ni msimu wa Harusi katika kipindi hiki cha pasaka, maonyesho haya ya Harusi si yakukosa kwa familia, marafiki,na wanakamati wa Harusi.huu ni wakati wa kupata vipaji vya ubunifu katika mambo yote ya Harusi.
Maonyesho ya Harusi 2012 ni bure kwa watu wote kuhudhuria
Maonyesho ya Harusi 2012 yamedhaminiwa Clouds FM, Clouds TV, The Citizen, Global Outdoor Systems, 2M Media, Ultimate Security, Vayle Springs, Eventlites, MH Gallery, Dar411, Epidor na 361 degrees.
0 comments:
Post a Comment