Pages

Sunday, September 23, 2012

PICHA 40 ZA USIKU WA MITINDO (MITINDO NIGHT), WAONE 'MAMODO' WALIVYOKONGA NYOYO ZA WATAZAMAJI MBALAMWEZI BEACH, USIPIME!!



MC katika maonyesho hayo alikuwa ni Ireene Tilya ambaye ni Mtangazaji wa Toneradio



















 Mkuu wa Operesheni wa Tone Mult-Media Company Limited Sillas Mbuya




 Mtangazaji wa Toneradio Kid Bwoy








 Head of Corporate Affairs wa Tone Mult-Media Company Limited, Victor Luvena (kushoto) akiwa na Afisa Masoko wa Tone Harold Mwakasala wakati wa maonyesho ya mitindo ya mavazi yaliyofanyika Septemba 22, mwaka huu pale Mbalamwezi Beach.



Wabunifu wa mavazi katika usiku wa mitindo uliofanyika Mbalamwezi beach walikuwa ni Diana Magese, Mitindonite iliwakilishwa na Ally, Amin, Wancy na Matrida, Bambo collection, Renee, Cocoriko, William Johnson, Veronica Ruhenzi-VS collection, Dorcas, Subira, Salim Ally, na Wavisa Collection.
Wengine ni Onfe collection, Baby Jullieth Collection na Hamidi Abdul collection. 
Maonyesho ya mitindo ya mavazi, yameandaliwa na Mitindonite Afrika na kudhaminiwa na Darling, Equity Bank, Tone Mult-Media Company Limted ambao ni wamiliki wa Tone radioBlogs za mikoa na Thisday Magazine, Secret Lengerie wauzaji wa nguo za ndani za wanawake, Amaya Beauty Solon & Spa, Better service, small axe, Qice photo sport, Real Burger, Fashion News, Pekuatanzania na Mdee Trans.
Blogzamikoa

Saturday, September 22, 2012

TBL YAKABIDHI MABASI YA KISASA KWA SIMBA NA YANGA

 Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akicheza sambamba na mashabiki wa timu hiyo wakionesha furaha yako baada ya Kampuni ya Bia Tanzania TBL kuvikabidhi klabu za Simba na Yanga mabasi mapya katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche  kulia akimkabidhi mfano wa ufunguo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga wakati wa hafla ya kukabidhi basi jipya kwa klabu hiyo. TBL ndio mdhamini Mkuu wa klabu za Simba na Yanga.
 Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche kama ishara ya makabidhiano ya basi jipya lililotolewa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam 
 Viongozi wa Simba na Yanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa TBL
Mkuu wa Usambazaji wa TBL, James Bokella akionesha ishara ya kuanza rasmi kwa msafara wa kuyatembeza magari ya Simbana Yanga katika mitaaya jiji la Dar es Salaam ili mashabiki wa timu hizo wayaone.

JK amteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa mkuu wa JKT

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba  (pichani kushoto) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali. Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman  A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
            
Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (pichani kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012. 
    

  Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali. Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012