Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi Jana mjini Arusha katika safari ya mwisho ya msanii wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava)Abeili Motika almaarufu kwa jina la Mr. Ebbo ambaye amezikwa kwenye makaburi ya ukoo nyumbani kwa mzee Lotiko.
Wananchi hao ambao walikuwa na shauku ya kuuaga mwili wa marehemu huyo walijitokeza kwa wingi huku wakionekana kuwa na nyuso za majonzi, kila mmoja akihuzunika na wengi wakidai kuwa mwimbaji huyo wa bongo flava ameacha pigo kubwa kwa jamii ya kimasai na Taifa kwa ujumla kwani muziki wake sambamba na kuburudisha ulikuwa unaelimisha kwa kiwango kikubwa.Akiongea katika mazishi hayo askofu mkuu wa jimbo la kaskazini Thomas Laizer alisema kuwa wao kama kanisa limeupokea msiba huo kwa masikitikio makubwa kwani msanii huyo alikuwa anaelimisha jamii kupitia nyimbo zake pia aliweza kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na kabila la kimasai kupitia nyimbo zake.
Habari kwa hisani ya Gsengo Blog.
MAY HIS SOUL R.I.P
0 comments:
Post a Comment