Pages

Thursday, October 6, 2011

msanii kutoka nigeria,mr flavour kunogesha shindano la bongo stars search second chance.!

MSANIII wa muziki kutoka nchini NIGERIA N’ABANIA maarufu kama MR FLAVOR anayetamba na kibao chake cha ASHAWOO katika vituo mbali mbali vya redio nchini atatumbuiza katika fainali za shindano la BONGO STARS SEARCH SECEOND CHANCE litakalofanyika tarehe 14 mwezi huuu katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE.

Mkurugenzi wa BENCHMARK PRODUCTIONS ambao ndio wa ratibu wa shindano hilo RITHA PAULSEN amesema kuwa msaniii huyo atatua nchini tarehe 12 akitokea nchini NIGERIA tayari kwa onyesho hilo litakalokuwa la aina yake.

RITHA amesema kuwa washiriki wanne tu ndio watakaochuana vikali katika kumsaka mshindi wa shindano hilo atakayejinyakulia shilingi milioni 40, mshindi wa pili milioni 10 na mshindi wa tatu milioni 5.

Tiketi za onyesho hilo zitaanzwa kuuzwa tarehe 11 mwezi huu ambapo zitauzwa katika vituo vya ,maduka ya SHEAR ILUUSION,BEUTY POINT,BIG RESPECT KARIAKOO,MANYWELE ENTERETIMENT,STEEERS na DIAMOND JUBILEE.

Amewataja washiriki hao ni pamoja na WAZIRI SALUMU MWENYE NAMBA BSS 23,ROGERS LUCAS BSS 27,BELA KOMBO BSS 05 na HAJI RAMADHANI BSS 11.

1 comments:

Anonymous said...

this is awesome i cnt miss the show ouchhh