Pages

Wednesday, October 12, 2011

Burudani kupamba Tusker Malt ‘Dar es Salaam Quiz Nite’

Meneja wa bia ya Tusker na Tusker malt za Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Rita Mchaki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)Dar es Salaam leo juu ya uzinduzi wa tukio la kiburudani linalojulikana kama ‘Dar es Salaam Quiz Nite’ litakalofanyika Hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam Oktoba 21 mwaka huu ambapo pamoja na burudani litahusisha mashindano ya vikundi kuhusu elimu ya kawaida ya kijamii.


Na Mwandishi Wetu.

KINYWAJI cha Tusker Malt cha Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kinatarajia kuzindua tukio jipya litakalopambwa na burudani kwa watu wa rika la kati linalojulikana kama Dar es Salaam Quiznite litakalofanyika Oktoba 21 mwaka huu katika hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam.

Tukio hilo litakalohusisha burudani mbalimbali ikiwemo ya muziki wa dansia litafanyika katika kila kipindi cha robo mwaka ambapo litahusisha washiriki wa rika la kati kutoka sekta mbalimbali za kiuchumi likiwa na lengo la kuwaunganisha na kushiriki katika burudani kwa pamoja na kubadilishana mawazo.

Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu tukio hilo Meneja wa kinywaji hicho Rita Mchaki alisema Tusker Malt kwa pamoja na wadau wengine wanashiriki katika tukio hilo ambapo taarifa zaidi ya burudani na matukio mengine yatakayojiri siku hiyo yatatangzwa baadaye.

Alisema Tusker Malt kwa pamoja na wadau wengine wanashiriki katika tukio hilo katika kutoa nafasi kwa wanywaji wao kuweza kupata uwanja mpana zaidi wa kuwa pamoja na kujenga mahusiano ya karibu kwa kushiriki burudani ya pamoja.

“Hii ni nafasi nyingine kwa wanywaji wetu kupata wigo mpana wa kuwa karibu na kinywaji cha Tusker Malt katika burudani ambayo itawasaidia kujenga mahusiano baina yao na marafiki zao ndani ya sekta tofauti”, alisema Mchaki .

Mratibu wa Tukio la burudani la ‘Dar es Salaam Quiz Nite’ kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Suzan James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo juu ya uzinduzi wa tukio hilo litakalofanyika Hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam Oktoba 21 mwaka huu ambapo pamoja na burudani litahusisha mashindano ya vikundi kuhusu elimu ya kawaida ya kijamii.


Uwanja wa ushiriki katika tukio hili unagusa nyanja mbalimbali ambapo vijana wa rika la kati wanaalikwa kushiriki bila masharti yoyote. Kwa upande wake Mratibu wa tukio hilo Suzan James kutoka SBL alisema Tusker Malt inaamini kupitia uwanja wa majadiliano kama huo , wanywaji watakuwa na nafasi nzuri ya kujifunza kutoka kwa wengine ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kufahamiana na wakati fulani kupanua soko la biashara.

Tukio hili la kipekee katika uwanja wa majadiliano litahusisha majadiliano ya vikundi vya watu kumi vikihusisha nyanja mbalimbali ambapo baadhi yake ni chapa za vitengo tofauti ,filamu, michezo ya kimataifa, muziki, sauti mbalimbali , watu maarufu na nyinginezo.

Zawadi mbalimbali za wazi zitatolewa kwa makundi washiriki ambapo sh. 1,000,000/- itakwenda kwa kikundi mshindi.“Kwahiyo natoa wito kwa wadau wote kutoka maeneo mbalimbali kuja na kushiriki katika tukio hilo la aina yake ya burudani na kufahamiana la Quiznite oktoba hii”, alisema James.

0 comments: