Pages

Friday, February 17, 2012

MAHAKAMA YA MAREKANI YAMHUKUMU KIFUNGO CHA MAISHA JELA RAIA WA NIGERIA ANAYETUHUMIWA KUJARIBU KULIPUA NDEGE YA ABIRIA.


Mahakama ya shirikisho mjini Detroit nchini Marekani imemhukumu mtuhumiwa wa shambulizi la bomu lililokuwa limefichwa kwenye nguo ya ndani ambaye ni mzaliwa wa Nigeria Umar Farouk Abdulmutallab (Pichani) adhabu ya kifungo cha maisha gerezani kwa kujaribu kuilipua ndege ya abiria wakati wa sikukuu ya Krismasi mwaka 2009.

Abdulmutallab mwenye umri wa miaka 25 na mtoto wa kiume wa mfanyakazi wa zamani wa benki raia wa Nigeria, anakabiliwa na mashitaka nane yakiwemo ya ugaidi kwa kujaribu kulipua ndege iliyokuwa na abiria wapatao 300 kutoka Amsterdam nchini Uholanzi ikielekea Detroit katika jimbo la Michigan nchini Marekani.

Hata hivyo bomu alilokuwa amelibeba kwenye nguo yake ya ndani halikulipuka kama ilivyopangwa.

0 comments: