Pages

Tuesday, January 10, 2012

MUSTAFA HASSANALI NA JERRY SILAA KUCHANGISHA MISAADA

Mbunifu wa kiafrika Mustafa Hassanali na Meya wa manispaa ya ilala Mh.Jerry Silaa wameungana kwa pamoja ili kuchangisha pesa kwa ajii yakuwasaidia watanzania waliokumbwa na janga la mafuriko lilosababishwa na mfululizo wa mvua kubwa ivi karibuni December 2011 jijini Dar es Salaam.

Maonyesho ya mitindo ya kwanza nchini Tanzania kufanyika kwa ajili ya kuchangisha pesa za kuwasaidia wahanga wa mafuriko,ambayo yatafanyika Alhamisi tarehe 12 Januari 2012 katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. Mustafa Hassanali ataonyesha ubunifu wake uliokubalika kimataifa kuanzia Johannesburg mpaka Stockholm,katika tukio hili tutaona wanamtindo wakitanzania wakiudhibitisha ubunifu wake.

“Nimeguswa sana na tatizo hili lilowakumba watanzania wenzetu, na kwa namna moja au nyingine wote tumeadhirika na tatizo hili. Ndo kwasababu mimi na Meya tumeamua kusaidia kwa kuandaa hafla ya kuchangisha pesa ya kuwasidia wahanga hawa”. Alisema Mustafa Hassanali

Mafuriko haya yameadhiri nchi nzima kiujumla, Mamia ya watu walokumbwa na janga hili la mafuriko hawana makazi ya kudumu na wengi wao wakiwa wanategemea misaada kama hii ili kujikimu katika mahitaji yao ya kila siku.

“Nngependa kuwahamasisha watu wengi waloguswa na tatizo hili kuhudhuria katika maonyesho haya ili kuweza kuwa mmoja kati ya watu watakaowasaidia na kuwafariji wahanga hawa wa mafuriko kwa kushirikana pamoja na kuleta mabadiliko katika maisha yao .” Alimalizia Hassanali.

Mitindo kwa ajili ya mafuriko yatafanyika katika hoteli ya Serena tarehe 12-Jan-2012 kuanzia saa 2:30 usiku, kiingilio ni shillingi 25,000 kwa viti vya kawaida na 50,000 kwa viti maalum . Maonyesho haya yamedhaminiwa na Serena Hotels Dar es Salaam, Clouds FM, Clouds TV, Vayle Springs, Event Lites, Darling Hair, H-Models, Samaki Samaki, Rockers night club, 24HR Media na 361 Degrees.


KUHUSU MUSTAFA HASSANALI

Mustafa Hassanali ni mbunifu mjasiriamali anaeamini katika ‘daima sitashindwa’ huku akitumia kipaji chake na ubunifu wake wa mavazi katika kuleta maisha bora ya sasa na ya baadae.
Kazi za mbunifu Mustafa zimekuwa zikithaminika na kuonyeshwa kimataifa, ambapo Mustafa alifanikiwa kuonyesha ubunifu wake katika nchi kama,Sweden,Niamey;FIMA, Angola ‘Angola Fashion Business’, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Kameruni, Wiki ya Mitindo India 2009, Naomi Campbell’s fashion for relief 2009, Arise Africa Fashion Week 2009, Wiki ya mavazi Durban & Cape town, Vukani Fashion Awards Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival, Sicily, Italia, M’net Face of Africa, Msumbiji, Uganda, na Wiki ya Mitindo Kenya, ambayo kwa pamoja yamemletea heshima kubwa, ndani na nje ya nchi.
Ukikutana na Mustafa Hassanali ndipo utajua uwezo wake utokanao na kazi zake,yeye kama yeye anajiamini katika kila anachokitengeneza na anatumia karama na ubunifu wake kutengeneza kilicho bora leo na hata kesho,hasa katika swala zima la mavazi, kwasababu kila akifanyacho hutoka moyoni. Mustafa ni Fashionista wa kweli ndani na nnje
Kwa habari zaidi tembelea tovuti www.mustafahassanali.net

Amisa Juma PR and Media Manager PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania 105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania (opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy) Tel : +255 (0)22 266 8555 Mobile : +255 (0)718735167 Networking : www.twitter.com/swahilifashion Web : www.mustafahassanali.net www.swahilifashionweek.com www.harusitradefair.com www.twende.info www.liveyourdreamstz.com www.fashion4health.org www.361.co.tz

0 comments: