Pages

Wednesday, November 30, 2011

Ngoma Africa Band Kuvamia Munchen Jumamosi Disemba 3



FFU wa Ngoma Africa Band kutoa burudani ya kukata na Mundu
Watanzania wanaoishi Ujerumani ! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru ! Kuanzia München hadi Berlin Chereko !Chereko! Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!
Watanzania waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona,sherehe hizo zinaanzia mjini München siku ya 3 Dec 2011 ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za Tanzania,mavazi,na mdahalo rasmi na usiku kutakuwa na muziki wa Ngoma Africa Band katika mtaa wa Siebold Str,11 ndipo penye ukumbi. Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio mji mkuu wa Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi wa UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja huo unawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na Bi.Tullalumba Mloge (katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin, UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU ! sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com

0 comments: