Pages

Wednesday, October 12, 2011

TDL yaandaa bonanza la kumpatia tuzo Mkongwe Maalim Gurumo

Muhidini Maalim Gurumo
Na Mwandishi wetu


KAMPUNI ya Tanzania Distillers Limited (TDL) Ijumaa itafanya bonanza la kumzawadia mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Gurumo katika viwanja vya Leaders Club.


Mratibu wa tamasha hilo, Mohamed Pizzaro amesema leo kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na mkurugenzi mtendaji wa TDL, David Mgwasa ndiye atakayetoa tuzo hiyo kwa Gurumo kama sehemu yake kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.


Pizzaro alisema kuwa Gurumo alianza muziki miaka ya 50, lakini alianza rasmi muziki wa jukwaani mwaka 1961 akiwa na bendi ya Kilimanjaro Chacha ambapo mwaka 1963, akajiunga na Kilwa Jazz.


Alisema kuwa baada ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wafanyakazi (NUTA), Gurumo akawa mwanamuziki wa kwanza kujiunga na bendi hiyo ambayo alidumu nayo mpaka mwaka 1978 alipojiunga na DDC Mlimani Park ‘Wana Sikinde Ngoma ya Ukae’ ambayo alihama mwaka 1986 na kujiunga na Orchestra Safari Sound (OSS)‘Wana Ndekule’.


Alifafanua kuwa Gurumo alirejea Msondo mwaka 1990 ambapo tokea ajiunge huko, hajahama tena.
“Zawadi gani atakayokabidhiwa, hiyo inajua kampuni ya TDL na Mgwasa mwenyewe, lakini ni ‘surprise’ kwa mashabiki na Gurumo mwenyewe,” alisema Pizzaro.


Alisema kuwa shamrashamra za tamasha hilo ambalo pia litakuwa la kumuenzi marehemu Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere litatumbuizwa na bendi ya Msondo baada ya mechi mbili za timu za maveterani.


Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Kigamboni na Namangan a mechi ya pili itakuwa kati ya Brake Point (BP) na Mango Garden.

0 comments: