Pages

Monday, October 17, 2011

NIMEJIANDAA VIZURI NA MASHINDANO YA MISS WORLD NAOMBA WATANZANIA WOTE MNIOMBEE NIWEZE KUSHINDA TAJI HILO -SALHA

WAKATI mwakilishi wa Tanzania katika shindano la urembo la Dunia (Miss World 2011) Salha Israel, anatarajiwa kuondoka keshokutwa kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kushiriki fanali hizo, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali wamemchangia zaidi ya shilingi milioni nane ili zimsaidie katikamaandalizi yake.


Akizungumza jana katika hafla ya kumkabidhi bendera mrembo huyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba alisema kwamba wafanyakazi na wadau mbalimbali wa serikalini wamejitolea fedha hizo ili kumpa sapoti katika kuelekea kwenye mashindano hayo.


“Nenda kwa kujiamini mrembo wetu nina imani kuwa utafanya vizuri katika mashindano hayo, tunafahamu kuna ushindani mkubwa lakini tunajua umejindaa vizuri, nenda katangaze vema utalii wa ndani wa nchi pamoja na vivutio, tupo nyuma yako kwa sala,”Alisema Mfutakamba


“Wizara imekuchangia dola 1000,mimi ninakupa shilingi mil.moja,kituo cha uwekezaji (TIC)dola 2000, pamoja na shilingi mil.3.4 nyingine toka kwa wafanyakazi wa wizara na wadau,”Alisema.


Naye mrembo huyo aliswhukuru kwa michango hiyo na kusema kuwa anakwenda kushiriki na si kushindana hivyo atatuamia vema mafunzo aliyoyapata toka kwa wakufunzi mbalimbali ili kuhakikisha anafanya vema katika mashindano hayo.


“Nimejiandaa vizuri na mashindano ya Miss World hivyo nawaomba Watanzania wote mniombee ili niweze kushinda taji hilo,”Alisema.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo fupi iliyofanyika mchana wa leo katika viwanja vya ofisi ya Kituo Cha Uwekezaji 'TIC' Jijini Dar es Salaam.


Fainali za Miss World zinatarajiwa kufanyika Desemba 3 huko London, Uingereza ambapo huu ni mwaka wa 18 Tanzania inawakilishwa katika fainali hizo huku Miss Tanzania wa mwaka 2005, Nancy Sumari ndiye aliyeweza kufanya vema ambapo alitwaa taji la Miss World Afrika.

Habari kwa hisani ya kamati ya maandalizi

0 comments: