Kinywaji cha Redd’s Original kinachotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kesho kitafanya tamasha lake la kwanza kwa wabunifu na wanamitindo wa vyuo vya Dar es Salaam. Tamasha hili lijulikanalo kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” lilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi October likiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya wabunifu na wanamitindo walioko katika vyuo vya elimu ya juu.
Akizungumzia tamasha hilo linalotarajiwa kuwa la kipekee na lenye mvuto mkubwa, meneja wa kinywaji cha Redd’s Bi. Victoria Kimaro alisema; Kesho (Jumamosi) tarehe 29, ndiyo ile siku tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu
kubwa. Tutakuwa na fainali za tamasha la Redd’s Uni – Fashion Bash kwa vyuo wa Dar es Salaam litakalofanyika katika ukumbi wa FPA Uliopo chuo kikuu cha Dar Es Salaa karibu na Benk ya CRDB (Udsm) hapa Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni na
kuendelea.
Maandalizi yote ya tamasha hili ambalo limeandaliwa kwa umakini wa hali ya juu ili kuonesha utofauti na matamasha yaliyozoeleka yemeshakamilika, na tutakuwa na washiriki kumi katika nyanja ya ubunifu (designers) watakoonesha kazi zao, pia tutakuwa na wanamitindo (models) ishirini watakao vaa mavazi ya wabunifu hao na kupita nayo jukwaani.
Redd’s Original pia imeandaa burudani za kutosha ili kunogesha tamasha hilo, ambapo wasanii Roma Mkatoliki na John Makini watatoa burudani ya kutosha, pia nawakumbusha wanavyuo wote kuwa tamasha hili halina kiingilio, hivyo ni ruksa kwa vyuo vyote vya hapa Dar es Salaam kuja kushuhudia vipaji vya wanavyuo wenzao na kupata burudani, alisema Bi. Victoria.
0 comments:
Post a Comment