Pages

Wednesday, October 19, 2011

MISS UNIVERSE TANZANIA 2011 NELLY KAMWELU KUELEKEA CHINA KUSHIRIKI MISS INTERNATIONAL 2011

Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu


Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu anataraji kuondoka leo mchana kuelekea mji wa Chengdu nchini China kwa ajili ya mashindano ya Miss International 2011.

Mrembo huyo atakuwa huko kwa kipindi cha wiki tatu ambapo mashindano yataanza tarehe 20 Oktoba na fainali zitakuwa tarehe 6 Novemba.

Nelly anaondoka akiwa amejiandaa ipasavyo kushiriki mashindano hayo ikiwemo mavazi mbalimbali yenye asili ya kitanzania kutoka kwa wabunifu wa hapahapa nyumbani. Akiwa huko atashindana katika mavazi mbalimbali ikiwemo vazi la jioni, vazi la taifa ambalo limebuniwa na Diana Magesa na vazi la ufukweni ambalo limebuniwa na Vida Mahimbo.

Mbali na mavazi lakini pia watawania tuzo ndogondogo kama vile talent(kipaji), mvuto katika picha (Miss Photogenic) na mahusiano mema(Miss Congeniality)

Nelly Kamwelu anakwenda huko baada ya kutoka katika mashindano ya Miss Universe hivi karibuni ambapo alishinda katika vazi la taifa na kushika nafasi ya saba ya mavazi. Vazi hilo pia lilibuniwa na Diana Magessa wa Morogoro.

Nelly anaondoka mchana wa leo na ndege ya Qatar airways.

0 comments: