Pages

Saturday, October 8, 2011

Balozi wa Kenya nchini Tanzania azindua mashindano ya kenya airways golf safari 2011 leo jijini dar

Balozi wa Kenya nchini Tanzania Matiso Mutinda akipiga mpira wa Gofu wakati akizindua Mashindano ya Kenya Airways Golf Safari kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam leo, huku Meneja mkazi wa Kenya Airways Lucy Malu wa tatu kulia akishuhudia, mashindano haya yanafanyika nchi zote za Afrika ambazo kampuni hiyo ina matawi, na mwakani washindi wote kutoka nchi 35 za Afrika watakutana pamoja mwakani na kuchuana jijini Nairobi nchini Kenya, ambapo mshindi wa kila nchi wa shindano hilo atagharamiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na malazi kwenda kwenye mashindano hayo makubwa nchini Kenya.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutindo Mutiso kulia akizungumza na Menenja Mkazi a kampuni ya ndege,Kenya Airways,Lucy Malu wakati wa uzinfunguzi wa mashindano ya Kenya Airways Golf Safari.
Meneja mkazi wa Kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lucy Malu akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa gofu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL), wakati wa uzinduzi wa Mashindano hayo ya Gofu yanayoitwa Kenya Airways Safari Golf, yanayozinduliwa leo katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa gofu Mustafa Jacks akipiga mpira wakati wa mashindano hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar mapema leo mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mchezaji K. Mbaya kutoka nchini Kenya akijiandaa kupiga mpira katika mzunguko wa kwanza wa mchezo huo.
Victor Joseph akipiga mpira.
Mwanadada Halima Mussa ambaye ni mmoja wa washiriki katika mashindano hayo ya Kenya Airways Golf Safari akijipinda vilivyo.
Meneja mkazi wa Kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lucy Malu katikati na Mchezaji wa gofu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL) wa pili kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa Kenya Airways mapema leo asubuhi ndani ya viwanja vya Gymkana,jijini Dar.
Wafanyakazi wa kampuni ya Blackberry Enterprises wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Michuzi Jr.


0 comments: